skip to Main Content

MLELE

Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga amewahakikisha Walimu mazingira rafiki ya uendaji kazi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao waliyopewa na serikali.

Mwanga ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Wadau wa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kilichoketi kwenye ukumbi wa Mikutano ukumbi wa Ukonongo kujadili mstakabali wa elimu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.

Aidha Mwanga amewahakikishia ushirikiano walimu na kusema hayuko tayari kusikia Kiongozi yeyote katika Wilaya yake akiwanyanyasa na kuwagombeza walimu.

Katika hatua nyingine amewaasa walimu kuendelea kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa ili kuleta maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mlele Teresia Irafay akiwasilisha Mkakati wa Elimu amewaeleza wadau wa elimu lengo ni kujadili Mstakabari wa elimu Halmashauri ya Mlele huku akiainisha changamoto zinazoikabili sekta ya elimu Mlele ikiwemo utoro wa wanafunzi,ubakaji, ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni.

Back To Top