Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kuacha mila potofu ya kufuata huduma za matibabu kwa waganga wa kienyeji badala yake wajenge tabia ya kuvitumia vituo vya kutolea huduma za afya vinavyojengwa na serikali katika maeneo yao .
Wameyasema hayo walipokuwa wanazungumza na Mpanda Radio Fm katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda walipokuwa wakipatiwa matibabu na kusema kuwa si vizuri kuendelea kuendekeza tamaduni za kuwaamini waganga wa kienyeji badala yake jamii inapaswa kufuata huduma za afya katika vituo vya afya.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Paul Nswakala amesema kuwa kwa sasa huduma za afya katika Manispaa ya Mpanda zimeimarika hivyo wananchi wanapaswa kuzitumia huduma hizo.