skip to Main Content

MPANDA

Mtu Mmoja aliyefahamika kwa jina la Elizabeti Fabiano mwenye umri wa mika 29 mkazi wa Mtaa wa shanwe Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi amefariki Dunia Kwa kuangukiwa na nyumba

Akizungumzia tukio Hilo mama mzazi wa marehemu Khadija Eneliko amesema mtoto wake amefariki Dunia baada ya kuangukiwa na Ukuta wanyumba usiku wa kuamika taerehe 16 ya mwezi huu walipokuwa wamelala.

Nao baadhi ya majirani wa mtaa wa Shanwe wamezungumzia namna walivyoguswa kutokana na tukio Hilo.

Lazaro Saimon Takamba Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Shanwe amekiri kutokea Kwa tukio hilo nakueleza kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia tarehe 16 mwezi huu wakati mvua iliyoambatana na upepo mkali ikiwa inanyesha huku akiomba serikali kutoa msaada kwa wahanga wa tukio hilo.

Back To Top