skip to Main Content

Picha na Mtandao

Utafiti uliofanyika wamegundua kuwa watoto  wenye umri wa miaka sita hadi tisa ndio waathirika Wakubwa

Na Samwel Mbugi -Katavi

Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni  mseto kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya afya ya kinywa na meno ambapo wameonyesha kutokuwa na  elimu ya kutosha ya namna ya utunzaji wa kinywa na meno

Hayo yamebainishwa na wananchi wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm wamesema kuwa hawana elimu ya Afya ya Kinywa na Meno ambapo wameitaka mamlaka husika kuendelea kutoa elimu kila wakati bila kusubiri siku ya maadhimisho.

Kwa upande wake Daktari  anayehusika na afya ya kinywa na meno Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Rhoda Mwakasege amesema kuwa utafiti uliofanyika wamegundua kuwa watoto  wenye umri wa miaka sita hadi tisa ndio waathirika zaidi kwa kiasi kikubwa.

Pia amewataka wananchi kutokukimbilia kutoa meno bila kufanya matibabu kwani kutoa meno inatakiwa kuwa  hatua ya mwisho baada ya matibabu kushindikana.

Ikumbukwe kuwa kilele cha maadhimisho ya Afya ya Kinywa na Meno kimefanyika tarehe 20 mwezi wa tatu mwaka huu, kwa kauli mbiu inayosema kinywa chenye furaha ni mwili wenye furaha.

Back To Top