“Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wananchi wilayani humo kuacha kujihusisha na na…
Baada ya Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania kutangaza kumvua uwakilishi wa Nchi kwenye mashindano ya Dunia, Miss Tanzania Rose Manfere mwenyewe ameibuka na kuwataka watanzania kusubiri uamuzi wa Baraza la Sanaa Nchini (Basata).
Rose ametoa wito huo kwa watanzania kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema mashabiki watulie kusubiri tamko la BASATA ili kujua mustakabali wake katika uwakilishi huo wa Nchi.
Kupitia Instagram akaunti yake Rose ameandika yafuatayo, ” Nimeona kupitia mitandao kwamba mshindi namba mbili wa Miss Tanzania atawakilisha Nchi kwenye mashindano ya Miss World, Mimi kama Miss Tanzania 2020/21 sina taarifa rasmi.”
Awali akizungumza na Michuzi TV, Mmoja wa wajumbe wanaounda kamati ya Miss Tanzania, Rico amesema kwa sasa hawana taarifa rasmi ila kuna baadhi ya kanuni na sheria ambazo Miss Tanzania anatakiwa kufuata na kusaini mikataba.
“Kwa kawaida Miss Tanzania anapovikwa taji kuna sheria na kanuni huwa zinamuongozo kipindi chote anapokua kwenye taji hilo hivyo ikitokea amekiuka mikataba inalazimika mshindi wa pili wa Miss Tanzania anapewa baraka zote za kushiriki mashindano ya Dunia (Miss World).