skip to Main Content

7 March 2024, 1:55 pm

“Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amesema mtuhumiwa alifikishwa mikononi mwa Jeshi hilo akiwa na hali mbaya hivyo muda mchache baada ya kufikishwa hospitali alifariki dunia na mwili kukabidhiwa kwa ndugu kwaajili ya mazishi” Picha na Deus Daud

Na Bertod Chove-katavi

Mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina moja la Christopher mwenye umri wa miaka 56 aliyekuwa akidaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka saba katika kijiji cha Dilifu kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amesema mtuhumiwa alifikishwa mikononi mwa jeshi hilo akiwa na hali mbaya hivyo muda mchache baada ya kufikishwa hospitali alifariki dunia na mwili kukabidhiwa kwa ndugu kwaajili ya mazishi.

Mbali na hilo jeshi la polisi mkoa wa Katavi limefanikiwa kukamata watuhumiwa 107 wanaojihusisha na makosa mbalimbali kati yao watuhumiwa sita wanajihusisha na mkosa ya mauaji.

Ngonyani amesema baadhi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali upelelezi unaendelea mara baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Back To Top