skip to Main Content

Wananchi amesema vitambulisho hivyo vitawasaidia kwani vimewaondoa hofu ya kukosa huduma muhimu ambazo zinaambatana na vitambulisho vya taifa kama vile kufungua akaunti za Benk Picha na Samweli Mbugi

Na Samweli Mbugi-katavi

Wananchi wa kata ya Mwamkulu Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wamefurahishwa na uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya taifa [Nida] kwa awamu ya pili uliofanya katika kata hiyo.

Wakizungumza na Mpanda Radio Fm wamesema kuwa vitambulisho hivyo vitawasaidia kwani vimewaondoa hofu ya kukosa huduma muhimu ambazo zinaambatana na vitambulisho vya taifa kama vile kufungua akaunti za Benk.

Wananchi wa kata ya Mwamkulu waliohudhuria katika halfla ya kukabidhi vitambulissho hivyo. Picha na Samweli Mbugi

Aidha Afisa usajili wa vitambulisho vya taifa Wilaya ya Mpanda Mauna Karumbeta wakati akisoma taarifa ya vitambulisho hivyo amesema kuwa wamepokea jumla ya vitambulisho 64,596 ambavyo vitagawiwa kwa kila kata huku zoezi hilo la ugawaji litasimamiwa na watendaji wa kata husika.

Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Mpanda ambae pia ni  mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya taifa Geofrey Mwashitete amesema kuwa kuna umuhimu kwa kila mwananchi apate kitambulisho cha taifa kwani kinafaida kwenye shughuli za kila siku.

Mwashitete ameongezea kwa kuwaagiza watendaji wote ndani ya Wilaya ya Mpanda kwa kutoa wiki moja kila mwananchi apate kitambulishio hicho huku zoezi hilo liendelee kusimamiwa na madiwani wa kata husika.

Back To Top