skip to Main Content

7 March 2024, 2:53 pm

“Matendo hayo ya huruma yamefanyika katika shule ya Msingi Nyerere na katika kituo cha kulelea Watoto yatima cha Yohana Paul wa pili Matumaini ya Watoto ambapo wamegawa mahitaji kama vile Madaftari , Mchele, na Juice” Picha na Lillian Vicent

Na Lilian Vicent-katavi

Kuelekea Maadhimisho ya siku ya Wanawake Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Sophia Kumbuli amewaongoza Wanawake kufanya matendo ya huruma kwa Wtoto wa Eimu maalumu pamoja na Watoto yatima

Matendo hayo ya huruma yamefanyika katika shule ya Msingi Nyerere na katika kituo cha kulelea Watoto yatima cha Yohana Paul wa pili Matumaini ya Watoto ambapo wamegawa mahitaji kama vile Madaftari , Mchele, na Juice .

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyerere Zuhura Kapama pamoja na Afisa Elimu maalumu wa Manispaa ya Mpanda Anna Sawasawa ametaka wazazi kuendelea kujitoa na kuwaibua watoto wenye ulemavu.

Nae mlezi wa kituo cha watoto Yatima Sista Rose Sungura amesema wanaojitokeza kusaidia watoto wanafanya hivyo kwa kuwa wanakujua wamewekeza kwa watoto hao.

Ikumbukwe kuwa maadhimisho ya siku ya Wanawake kwa mkoa wa Katavi yatafanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Mkurugenzi mtendaji wa halamashauri ya Manispaaa ya Mpanda( katikati Mwenye kitambaa) akiwa na watoto pamoja na wanawake manispaa ya mpanda baada ya kukabidhi mahitaji kwa watoto yatima na wenye mazingira magumu kituo ya masisita MPANDA

Back To Top