“Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wananchi wilayani humo kuacha kujihusisha na na…

Picha na Mtandao
“Jamii inapaswa kupewa elimu juu ya namna ya kumuinua mwanamke kiuchumi pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia ili kuwepo na usawa wa kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke“
Na Rachel Ezekia-Katavi
Umaskini umetajwa kuwa chanzo cha ukatili wa kijinsia kwa wanawake katika jamii na kupelekea ukandamizaji wa haki kwa kundi hilo.
Hayo yameelezwa na Wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ambapo wamesema uwepo wa mifumo dume na kutowapa fursa za kiuchumi Wanawake kunapelekea kuongezeka kwa matendo ya ukatili dhidi ya Wanawake.
Afisa ustawi wa jamii kutoka hospitali ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Malagano Thabiti amesema mifumo dume iliyopo katika jamii inapelekea kuongezeka kwa ukatili kwa jinsia kwa wanawake na kuwataka wanaopitia ukatili kujitokeza ili kupata msaada wa kisheria.
Jamii inapaswa kupewa elimu juu ya namna ya kumuinua Mwanamke kiuchumi pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia ili kuwepo na usawa wa kijinsia kati ya Mwanaume na Mwanamke.