miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
“Daktari wa Manispaa ya Mpanda Coronel Bruno amesema kuwa ongezeko la Ugonjwa huo inatokana na Wananchi kutokuzingatia kupima Afya kila mara ili kubaini.” Picha na Mtandao.
Na Veronica Mabwile-katavi
Baadhi ya Wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameiomba Serikali mkoani Katavi kuongeza jitihada za utoaji wa Elimu juu ya Magonjwa ya Kuambukiza ikiwemo Ugonjwa wa Homa ya ini ili kuongeza uelewa kwa Wananchi.
Wananchi hao wametoa ombi hilo kufuatia uwepo wa ongezeko la ugonjwa huo na kusema kuwa namna ya kutokomeza Ugonjwa huo ni pamoja na Wananchi kupewa elimu ya kutosha juu ya dalili za Ugonjwa huo na namna ya kujikinga.
Akizungumza Wakati wa kongamano la Wanawake daktari wa Manispaa ya Mpanda Coronel Bruno amesema kuwa ongezeko la Ugonjwa huo inatokana na Wananchi kutokuzingatia kupima Afya kila mara ili kubaini
Miongoni mwa dalili za ugonjwa wa homa ya ini ni pamoja na Mcho kubadilika rangi na kuwa ya Njano, kupungua Uzito, hamu ya kula ,pamoja na ngozi ya Mwili kuwasha.