Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
KATAVI
Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi wameaswa kuendelea kuhabarisha mambo yanayofanywa na serikali katika sekta Mbalimbali ili wananchi wafahamu namna serikali inanyo sogeza huduma hizo kwa Wananchi.
Deodatus Kangu Afisa utumishi wa Manispaa ya Mpanda aliye Mwakilisha Msitahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry kwenye Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari amesema kazi ya uandishi wa habari huleta ustawi wa Jamii kupitia Habari zinazoandikwa na kuleta Mtizamo chanya kwenye Jamii ili kuongeza uwajibikaji kwa Mamlaka zilizopo ili wananchi waweze kupata huduma.
Aidha Mwenyekiti wa Klabu ya wandishi wa habari mkoa wa Katavi walter Mguluchuma amewaasa waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.
Kwa upande wake Rais wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania Deogratius Nsokolo amesema kuwa anaishuru serikali ya awamu ya Sita kwa kukubali kuanza mchakato wa Ulekebishaji wa sheria za habari ambazo zilikuwa zinaoneka kuwa kandamizi kwa waandishi wa habari hapa nchini.
Nsonkolo amewakumbusha waandishi wa Habari kuendelea kuwa sauti ya watu wasio kuwa na sauti kwa kuibua changamoto zao ili serikali iweze kuwajibika kwa kupeleka huduma kwenye maeneo yenye changamoto za Maji,Elimu Afya na miundombinu.
Katika maadhimisho hayo ya Uhuru wa vyombo vya Habari waandishi wa Habari katika mkoa wa Katavi wamepata fursa ya kupatiwa elimu kuhusu habari zinazo husu Masuala ya kipolisi yaliyotolewa na maafisa kutoka jeshi la polisi mkoa wa katavi pamoja na Elimu kuhusu Madhara ya Rushwa yaliyotolewa na maafisa kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa katavi.