Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
KATAVI
Vijana mkoa wa Katavi wameaswa kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali kwa kuunda umoja na kusajiliwa kisheria na Bodi ya wakandarasi ili waweze kupata kazi zinazotolewa na serikali kupitia wakala wa Barabara Tanrods katika mkoa wa Katavi.
Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Tanrods Mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende ambapo amesema katika sera ya Wizara ya Ujenzi kwenye Bajeti za Mkoa Asilmia 30 Hutengwa kwaajili ya Makundi Maalamu ambayo ni Wazee,Wanawake ,walemavu na Vijana ambapo makundi haya huyalazimu kusajiliwa katika Bodi ya Wakandarasi na baadae hatua zingine za kuomba miradi hiyo hufuata.
Amesema katika Mwaka wa fedha ujao Tanroads katika mkoa wa Katavi wanatarajia kuwa na kazi ndogo ndogo 16 ambapo zitahusisha makundi hayo kwa kuangalia Mahitaji ya kazi kulingana na uhitaji katika miradi husika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jukwaa la kuwakomboa vijana Mkoa wa Katavi Saimon John amesema vijana wanatambua mchango wa Tanrods namna inavyoshrikiana na na jukwaa la vijana katika uelimishaji wa jamii unaofaywa na jukwaa la vijana kwa wananchi kwenye maeneo ambayo miradi hiyo ya Tanrods inapojengwa.
Katika hatua nyingine Jukwaa la kuwakomboa vijana mkoa wa Katavi limetoa cheti cha Shukurani Kwa ofisi ya Tanrods Mkoa wa Katavi kwa kutambua mchango unaotolewa na ofisi hiyo katika kwenye uelimishaji wa jamii kuhusu VVU na Ukimwi kwenye baadhi ya maeneo ambayo miradi mbalimbali ya ujenzi wa Barabara hufanyika.