skip to Main Content

TANGANYIKA

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu ametoa wito kwa wazazi kurudi enzi za nyuma kwa kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao badala ya kuwawekea katuni kwenye runinga huku watoto wakiendelea kuharibika kimaadili.

Buswelu ametoa wito huo katika maadhimisho ya Siku ya Familia duniani Kwa wilaya,yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ifukutwa, Halmashauri ya Tanganyika Mkoani Katavi.

Amesema yapo mambo yanafanywa na jamii yasiyompendeza Mungu kama mapenzi ya jinsia moja na vikiwemo vitendo vya ukatili, ukichunguza vinatokana na kukosekana kwa maadili hivyo ipo haja ya wazazi na walezi kuwatengenezea misingi mizuri watoto kabla hawajaharibika.

Akirejea maneno ya Mungu katika Biblia, Buswelu amesema Mungu alipoona matendo maovu yamekithiri katika uso wa dunia, alichukia na kushusha gharika na Sodoma na Gomora ikateketea na watu wote, na ameitaka jamii kuachana na matendo maovu kabla Mungu hajachukia na kushusha gharika.

Hassan Mapengo mkazi wa Tanganyika amesema zamani wazazi walikuwa na utamaduni wa kukutana na watoto tofauti na sasa ambapo wazazi hawana muda wa kuzungumza na watoto zaidi wanarudi usiku.

#mpandaradiofm97.0

#tanganyikadc

#ustawiwajamii

Back To Top