skip to Main Content

MPANDA

Jamii Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imetakiwa kuendelea kupinga vitendo vya ulawiti na Mapenzi ya jinsia moja sambamba na kuwapa malezi bora watoto wao ili waendelee kuwa na maadili mazuri.

Hayo yamejiri katika kikao cha baraza la madiwani ambapo Afisa Maendeleo ya jamii Marieta Mlozi ameeleza juu ya vitendo vya ukatili ambavyo watoto wanafanyiwa ikiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kueleza kuwa vitendo hivyo vinatokana na malezi yasiyofaa katika familia sambamba na vitendo vya ajira kwa watoto

Kwa upande wao baadhi ya madiwani waliohudhuria kikao hicho wameitaka jamii kupinga vikali vitendo hivyo kwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili wahusika wachukulie hatua.

#mpandaradiofm97.0

#mpandamanispaa

#TBCfm

#wasafifm

#efmtanzania

#cloudsfmtz

Back To Top