Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Wakulima wa mahindi katika Kijiji cha Sungamila kata ya Kasokola manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametaja mbolea ya msimu imewasababishia hasara katika kilimo hicho.
Wakizungumza na Mpanda Redio FM kwa nyakati tofauti wakulima hao wamesema kuwa katika msimu huu wa kilimo wametumia nguvu Kubwa lakini mbolea imekuwa kikwazo kutokana na kutoleta matokeo waliyotarajia.
Afsa kilimo manispaa ya Mpanda Gwalusa Kapande amesema kulikuwepo na changamoto ya mbolea kampuni ya Mijingu kwa wakulima waliotumia imeonekana tatizo kwa wakulima na kama serikali imefanya mawasiliano na Kampuni hiyo juu ya changamoto iliyojitokeza ili kubaini chanzo cha tatizo.
Aidha Kapande amewataka wakulima kuwa na desturi ya kuwasiliana na maafisa ugani ili kuondokana na changamoto hizo.