Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
NSIMBO
Wananchi wa kijiji cha Itenka A Halmshauri ya Nsimbo wamekumbwa na sintofahamu baada ya mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa uliopangwa kujengwa kijijini hapo kuhamishwa na kupelekwa kijiji jirani.
Wakizungumza na kituo hiki wananchi wamesema kuwa awali ulipangwa kujengwa kijijini hapo ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi lakini katika hali ya kusikitisha mradi huo umehamishwa na kupelekwa katika kijiji cha Tumaini.
Akijibia sintofahamu hiyo diwani wa kata ya Itenka Joseph Mpemba amekiri fedha zaidi ya Milioni 500 zimeingizwa katika akaunti ya kijiji kwa ajili ya ujenzi lakini wameamua kupeleka mradi huo katika kijiji cha Tumaini kitongoji cha Jilabela kutokana na uhaba uliokithiri wa vyumba vya madarasa.