skip to Main Content

MPANDA
Kata ya Kawajense na Nsemlwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa madawati na vyumba vya madarasa katika Shule za msingi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mpanda Radio fm diwani wa kata ya Kawajense Uwezo Bacho na diwani kata ya Nsemlwa Bakari Kapona wamesema Suala la madawati ni muhimu likawekewa mkazo kuanzia serikalini hadi kwa jamii ili kuwasaidia Watoto kujifunza kwa uhuru.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema kuwa upo mkakati wa kuwashirikisha wazazi ili kuongeza nguvu katika kuchangia madawati.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kuna upungufu wa madawati 900.

Back To Top