skip to Main Content

MPANDA
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusufu amewataka maafisa lishe na wadau kusimamia vyema na kutoa elimu juu ya lishe ili kuepukana na tatizo la udumavu na utapiamlo kwa watoto

Hayo yamesemwa katika kikao cha lishe cha robo ya kwanza kuanzia mwezi julay hadi september ambapo maafisa lishe wamesoma taarifa ya afya kwa manispaa ya mpanda Mwanaidi Salimu na halmashauri ya Nsimbo Nickson Yohanes ambapo wameanisha watoto ambao wamegundulika kuwa na utapiamlo.

Kufwatia taarifa hiyo mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusufu amewataka maafisa lishe na wadau mbalimbali kuhakikisha elimu inawafikia wananchi ili waelewe chakula kinachostahili kutumika kwa ajili ya lishe.

Sambamba na hilo mkuu wa wilaya, amewataka wataalumu kuwapa elimu wananchi ili waweze kutambua na kulima mazao ya chakula yanayosaidia kuleta lishe .

Kikao hicho cha robo ya kwanza kwa mwezi julay hadi september kimekuwa na ajenda mbili ikiwamo ajenda hiyo ya lishe pamoja na ajenda ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele ambapo chanjo zitatolewa za kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa hayo ikiwamo kichocho.

Back To Top