Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Mwaka wa fedha 2021/22, Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Katavi imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 7.2 sawa na asilimia 117.42 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 6.2.
Kamishina Mpelelezi wa Kodi TRA Makao Makuu, Andengenye Mwaipopo amesema makusanyo hayo ni ongezeko la Tsh. Bilioni 1.7 ikilinganishwa na kiwango cha makusanyo ya bilioni 5.4 kilichofikiwa mwaka 2020/21.
Jamila Yusuf Mkuu wa wilaya ya Mpanda kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Katavi ameipongeza Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Katavi kwa kuvuka lengo na ametoa wito kuhakikisha mafanikio hayo yanaamsha ari kufanya vizuri mwaka unaofuata katika ukusanyaji mapato
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Katavi, Amani Mahela amesema wataendelea kutoa ushirikiano kwa TRA na kuhakikisha wanakuwa waaminifu kwa kulipa kodi kwa wakati ili kuwafanya TRA Katavi kuendelea kuwa vinara.