skip to Main Content

KATAVI

Jumla ya Tofali Elfu kumi zimepokelewa  na kamati ya Ujenzi wa Shule ya Msingi Msasasani  iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule  Celestine Shemtange  ameiambia Mpanda Radio kuwa Tofali hizo zimetokana na Michango ya Wananchi ambao nguvu zao zinatakiwa kukamilisha maboma mawili.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mapokezi ya Vifaa katika ujenzi wa shule ya msingi Msasasi Juvenary Deus amewaomba wadau kuendelea kuchangia juhudi zinazofanywa na Wakazi wa Kata ya Mpanda Hotel ili kuweza kusaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi  katika shule zilizopo katika kata hiyo.

Aidha  Wananchi wa kata hiyo wameomba Wakazi wenzao kujitokeza kushirikiana na  na kushikamana kwa michango na kujitolea ili kuweza kufanikisha kunyanyua boma la shule hiyo.

Back To Top