skip to Main Content

MPANDA

Baadhi ya viongozi wa kikundi cha Kagera group wamevuliwa nyazifa zao kutokana na mgogoro unaoendelea katika kijiji cha Dirifu Na  wachimbaji wadogo huku nafasi zao zikitarajiwa kuzibwa hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa kutoa maamuzi hayo diwani wa kata ya Magamba Fortunatus  Chiwanga amesema kukosekana kwa nyaraka za maandishi walizoagizwa kagera group, wameshindwa kuziweka wazi mbele ya wananchi juu ya makubaliano baina yao na muwekezaji.

Akizungumza mtendaji wa kata ya Magamba RADISLAUS TABAN amesema kuwa wamejiridhisha kuwa kikundi cha kagera  waliingiia kuingia mkataba mpya na muwekezaji pasipo kuwashirikisha wananchi na serikali juu ya tozo zitakazo katwa kwa wachimbaji baada ya kukwangua mlima.

Wananchi wa kijiji cha Dirifu wamefurahishwa na uamuzi huo huku wakisema kikundi hicho kilitaka kuwageuka kwa kuingia mikataba ambao haina uwazi ambayo inadhaniwa ingekuwa kuwa na madhara kwao hapo baadae.

Back To Top