skip to Main Content

KATAVI

Wadau wa maendeleo Mkoani katavi wameombwa kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Makanyagio iliyopo Manispaa ya Mpanda.

Afisa mtendaji wa Kata ya Makanyagio Maiko Ndaile  amesema kuwa tayari wameanza ujenzi kwa michango ya wananchi wakishirikiana na Viongozi ndani ya Kata hiyo.

Nae Mwenyekiti wa mtaa wa kachoma Noel Ngomalufu Nsonkolo amesema kuwa wananchi wanaendelea kuhamasishwa katika kujitolea  kwa ajili ya  ujenzi wa zahanati hiyo ambayo imefikia hatua ya msingi katika ujenzi wake.

Awali akizungumza kwa  njia ya simu diwani wa kata ya makanyagio Haidary Sumry katika kuendelea kuhamasisha ujenzi huo ametoa Tofali za Bloko Elfu moja ambazo zimetumika katika ujenzi wa Msingi  huku akiendelea kutoa Wito  kwa  wananchi wa kata hiyo kuendelea kuchangia ujenzi wa Boma la Zahanati hiyo.

Back To Top