“Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wananchi wilayani humo kuacha kujihusisha na na…
“Wazazi wa marehemu Lwitiko hawatambua kama mtoto wao huyo aliwahi kubadili dini na kuwa mwislam“
Na Samwel Mbugi-Katavi
Familia ya marehemu aliyefahamika kwa jina la Lwitiko Bukuku imeiomba mahakama kutenda haki katika kesi iliyofunguliwa na anayejieleza kuwa ni mke wa marehemu akidai mumewe amezikwa kwa imani ya dini ya Kikristo badala ya imani ya Kiislamu.
Hayo yamesemwa na dada na kaka wa marehemu Mary Bukuku na Edward Bukuku wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm kuwa kesi hiyo imeleta taharuki kwa ndugu na jamaa kwani wao kama familia hawakujua kama marehemu alikuwa amebadili dini.Sauti za dada na kaka wa marehemu Mary Bukuku na Edward Bukuku
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mnazi mmoja Mussa Alfani amesema kuwa tarifa za ufukuaji wa kabuli ni za kweli na zilileta taharuki kwa wanachi wa mtaa huo kwani tukio hilo ni mara ya kwanza kutokea katika mtaa wake.Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnazimmoja akizungumza
Pia Mussa amewataka wananchi wanaomzushia kuwa ameegemea upande mmoja waache mara moja kwani yeye anasimamia haki ya kila mwananchi wa mtaa wake tofauti na wanavyofikilia kuwa yuko upande wa familia ya marehemu.Sauti ya Mwenyekiti Mtaa wa Mnazimmoja
Hata hivyo Mahakama ya wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi imekubali ombi la rufaa kwa ndugu wa marehemu ambayo imesikilizwa Aprili 29, 2024 ya zuio la kufukua mwili wa marehemu ambapo ulipaswa kufukuliwa na kuzikwa upya kwa imani ya dini ya Kiisilam ,na kesi hiyo itapangwa tarehe ya kusikiliza tena.