miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
MPANDA.
Baadhi ya wafugaji wa kuku manispaa ya mpanda mkoani katavi waishukuru kampuni ya silverlands kwa kuwapa mafunzo ya ufugaji kuku wenye tija.
Wameyasema hayo walipokua wakizungumza na mpanda radio fm mara baada ya mafunzo yaliyofanyika katika ofisi ya mtendaji kata ya kawajense na kusema kuwa wamepata elimu ambayo itaenda kuwaongezea kipato kupitia biashara hiyo na kuongeza uchumi katika familia zao.
Mwanamvua Ngocho ambaye ni meneja masoko wa kampuni ya silverlands amesema kuwa ni wakati wa wafugaji kufuga kibiashara kwa kupata vifaranga bora kutoka kampuni hiyo.Sauti ya Meneja Masoko Kampuni ya Silverlands
Silverlands ni kampuni inayozalisha vifaranga bora na chakula bora cha kuku ambapo makao makuu yapo mkoani Iringa.