skip to Main Content

KATAVI

Wakulima Mkoani  Katavi wameiomba serikali kuwapunguzia bei  ya  pembejeo za kilimo zikiwemo mbolea pamoja na mbegu.

Wakizungumza na Mpanda radio FM wakulima hao  wamesema ili waweze kuendelea kulima kwa faida na kwa haraka wanapaswa kupata pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu.

Kwa upande wake Afisa kilimo Mkoa wa Katavi amebainisha kuwa moja ya sababu zinazopelekea kupanda kwa pembejeo  ni uhitaji mkubwa katika soko la dunia.

 Hata hivyo amewataka wa kulima kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho serikali inashughulikia suala hilo.

Back To Top