skip to Main Content

WASHINGTON

Rais wa Marekani Joe Biden amesema amezungumza na Rais wa China Xi Jinping kuhusu Taiwan  baada ya China kutuma idadi kubwa ya ndege za jeshi katika anga ya taiwan.

Biden amesema katika mazungumzo yake na Xi, wamekubaliana kuheshimu makubaliano ya Taiwan, huku mivutano ikiwa imepamba moto kati ya mataifa hayo mawili ya Asia.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani, Ned Price, amesema Marekani inatiwa wasiwasi sana na shughuli za kijeshi za China karibu na Taiwan, ambazo zinatishia amani ya eneo hilo.

China inadai Taiwan kuwa ni eneo lake, na lina haki ya kulichukua kwa nguvu, huku Taiwan ikidai kuwa ni nchi huru na itatetea uhuru wake na demokrasia, na kwamba China ndiyo ya kulaumiwa kwa mivutano iliyojitokeza.

Back To Top