skip to Main Content

DAR ES SALAAM. 

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan ameelekeza kupunguzwa kwa tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali katika bidhaa za mafuta hapa nchini zenye thamani ya Sh102 bilioni kwa mwaka,.

Rais Samia ametoa agizo hilo   wakati akipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Nishati, January  Makamba kuhusu utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa Wizara hiyo kupitia mwenendo wa biashara ya mafuta na bei zake hapa nchini.

Taarifa iliyotolea na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imeeleza kuwa utekelezaji wa maagizo hayo unaenda sambamba na marekebisho ya kanuni mbalimbali zinazohusiana na tozo na kuchapishwa katika gazeti la Serikali Oktoba 05 ,2021.

Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Samia amechukua hatua ili kukabiliana na upandaji wa bei za mafuta katika soko la dunia, ambapo kwa muda mrefu imekuwa ikipanda kwa kiwango kikubwa na kuathiri watumiaji wa bidhaa hiyo hapa nchini.

Back To Top