skip to Main Content

Mrindoko akijibu kero hiyo amemtaka mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph kuhakikisha  wanalifuatilia swala hilo na kulipatia ufumbuzi ili mkulima afanya kazi yake bila changamoto yoyotePicha na Festo kKnyogoto

Na Samwel Mbugi-katavi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mwanamvua Hoza Mrindoko ameendelea na ziara ya kusikiliza kero za Wananchi kata ya Shanwe   mtaa wa Kivukoni  ambapo amekuatana  na  kero ya  wakulima mazao yao kuliwa na mifugo.

Akizungumza katika mkutano huo mmoja wa wakulima amesema kuwa baadhi ya wafugaji wamekuwa wakilisha mifugo katika mashamba yao kwa maksudi na kuwapelekea kupata hasara .

Mrindoko akijibu kero hiyo amemtaka mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph kuhakikisha  wanalifuatilia swala hilo na kulipatia ufumbuzi ili mkulima afanya kazi yake bila changamoto yoyote.

Mkuu wa wilaya ameomba kupewa muda kufuatilia swala hilo ili kuhakisha anamaliza migogoro kati ya wakulima na wafugaji wa maeneo hayo.

Ikumbukwe kuwa ziara hiyo ni mwendelezo wa Kliniki ya tuzungumze Live ambapo wananchi huwasilisha kero zao mbalimbali na kupatiwa ufumbuzi 

Back To Top