“Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wananchi wilayani humo kuacha kujihusisha na na…
“Kuna changamoto ya Ini na Figo kushindwa kufanya kazi, na Saratani kuongezeka katika Jamii Yanayosababishwa na matumizi mabaya ya dawa kwa baadhi ya Wananchi” Picha na Mtandao
Na Samwel Mbugi-katavi
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba [TMDA] kutoka makao Makuu Dodoma imetoa Elimu kwa Wananchi wa Misengereni kata ya Ilembo mkoani Katavi kuhusu matumizi sahihi ya dawa na utoaji wa taarifa za maudhi yanayotokana na matumizi ya dawa na vifaa tiba.
James Ndege Afisa mwandamizi wa TMDA amesema kuwa wamefanya utafiti na kubaini kuwa kuna changamoto ya Ini na Figo kushindwa kufanya kazi, na Saratani kuongezeka katika Jamii Yanayosababishwa na matumizi mabaya ya dawa kwa baadhi ya Wananchi.
Aidha Ndege amesema kuwa baadhi ya watu wanachanganya kwa wakati mmoja tiba ya Hospital na tiba Asili jambo linalopelekea kuchosha Figo na Ini ambapo baadhi ya wananchi huamini kuwa dawa za asilia hazina kemikali.
Kwa upande wa Wananchi wameshukuru kutolewa kwa Elimu hiyo ambapo awali walikua wanatumia dawa bila kufuata taratibu za kitabibu na Elimu hiyo imekuwa mkombozi.
Katika hatua nyingineJames Ndege ametoa wito kwa Wananchi wanaoenda kupata matibabu Hospital kuhakikisha matibabu wanayapata wanakamilisha dozi bila kuchanganya na tiba nyingine.