skip to Main Content

Picha na Mtandao

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema suala hilo lipo katika uchunguzi na hatua kali za kisheria zitachukuliwa huku wao kama serikali wamesikitishwa kutokea kwa tukio hilo”

Na Gadness Richard-katavi

Binti mwenye umri wa miaka 13 mkazi wa Kijiji cha Kawanzige kata ya kakese manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amebakwa na mfungwa wa gereza la kalilankulunkulu wakati alipokuwa anatoka mbugani kupanda mpunga.

Binti huyo ambaye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa  tukio hilo limetokea wakati alipotoka mbugani akiwa na wenzake ndipo mfungwa huyo akiwa anachunga ng’ombe aliwaamuru wasimame na baadae kufanya tukio hilo.

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa  Hospital ya manispaa ya Mpanda Limbu Mazoya  amesema kuwa walimpokea binti huyo na baada ya kumfanyia uchunguzi alionekana kuwa na viashiria vya kubakwa.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari amesema suala hilo lipo katika uchunguzi na hatua kali za kisheria zitachukuliwa huku wao kama serikali wamesikitishwa kutokea kwa tukio hilo.

Mrindoko amesema matukio ya ukatili yamezidi kuwa mengi huku akiwaomba wazazi na walezi kutokuyafumbia macho masuala ya ukatili na kuwataka  watoe taarifa pindi matukio kama hayo yanapojitokeza.

Back To Top