skip to Main Content

KATAVI

Baadhi ya madereva bajaji mkoani Katavi wameeleza namna ambavyo bima za vyombo vya moto haziwasaidii pindi yanapotokea majanga ya barabarani.

Wameyaeleza hayo wakati wakipewa elimu juu ya umuhimu wa bima za vyombo vyao vya moto ambapo wamesema aina hiyo ya bima haiwasaidii wao madereva badala yake inawasaidia wamiliki wa chombo na abiria au yule aliyesababishiwa ajari.

Kwa upande wake afisa bima kutoka shirika la bima la taifa Pili Salum ametolea ufafanuzi juu ya ukakasi wanaoupata madereva kuhusiana na bima hiyo kutowasaidia wao huku akieleza umuhimu wa bima ikiwa ni pamoja na kukinga na majanga ya barabarani.

Zoezi hilo la utoaji wa elimu ya bima kwa madereva wa vyombo vya moto bado ni endelevu mkoani hapa.

Back To Top