Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
TANGANYIKA
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kabungu kata ya Kabungu wilayani Tanganyika mkoani katavi wameiomba Serikali kuwaletea mkunga wa kike kwenye zahanati ya kijijini hapo.
Wakizungumza na mpanda radio fm wananchi hao wameipongeza zahanati hiyo kwa huduma wanazozitoa huku wakiomba waongezewe mkunga wa kike.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa zahanati ya hiyo Buchimi Nicodem amesema kuwa wananchi wasiwe na hofu kwani wauguzi hao wamebobea na wanatunza siri za wagonjwa.