Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
KATAVI
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametoa siku saba kwa wakurugenzi wa halmashauri, waganga wakuu walaya na maafisa lishe kutoa maelezo ya kina kwa maandishi kwa kushindwa kusimamia mkataba wa lishe.
Agizo hilo amelitoa wakati wa kikao cha kujadili tahtimini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe, mkakati wa kuzuia magonjwa ya mlipuko, na utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto mkoa wa Katavi amesema watendaji wengi hawawajibiki kutekeleza majukumu yao jambo ambalo linapelekea kutofikia malengo na mkakati iliyowekwa kwa wakati.
Afisa lishe mkoa wa Katavi Asinati Mlema amekiri kupokea maagizo hayo ya mkuu wa mkoa na kuhakikisha ndani ya siku saba taarifa rasmi inakamilika na kuwasilishwa kwa mkuu wa mkoa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Iddy Kimanta amesema suala la lishe ni mhimu ili kuepukana na udumavu na kupata kizazi bora cha baadae.