skip to Main Content

KATAVI

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani wanafunzi wa kike katika manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameaswa kutoa taarifa kila waonapo ukatili wa kijinsia.

Akisoma taarifa afisa maendeleo ya jamii manispaa ya mpanda bi Marietha Mlozi  amesema wanaiadhimisha siku ya wanawake kwa kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo hasa kutoa elimu kwa jamii.

Aidha akimuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Leah Gawaza akizungumza Mbele ya wanafunzi Pamoja na wanawake katika shule Ya sekondari ya  Rungwa iliyopo Manispaa ya Mpanda amewataka kuhakikisha wanatoa taarifa pindi yanapofanyika matendo yasiyofaa na kuwasisitiza wazazi kusimama  vyema  katika jukumu la malezi.

Wanafunzi wa shule hiyo ya sekondari rungwa wamesema wamepokea na watafanyia kazi yale waliyoambiwa sambamba na kutoa taarifa pindi watakapoona vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande mwingine wamepanda miti 400 katika eneo la shule hiyo kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo ufanyika march 8 Kila mwaka

Back To Top