skip to Main Content

KATAVI

Manispaa ya Mpanda imetoa mashamba kwa vijana ambao hawakuchaguliwa kushiriki  Mafunzo ya BBT-YIA (Building a Better Tommorow Youth initiative for agriculture ) yaliyo ratibiwa na wizara ya kilimo  na kutolewa  February  15 Mwaka huu jijini Dodoma.

Afisa kilimo, mifugo na uvuvi manispaa ya Mpanda gwalusajo Kapande amesema kuwa, manispaa imetoa mashamba hayo kwa vijana waliokosa nafasi ya kushiriki mafunzo ya kilimo kwa mwaka 2023, kwani ndani ya manispaa ni vijana nane tu ndio waliobahatika kupata nafasi hiyo.

 Aidha baadhi ya wananchi na vijana wameishukuru manispaa kwa mkono wizara ya kilimo kwa kutoa mashamba kwa vijana ambao hawajafanikiwa kupata kuchaguliwa kwenye mafunzo mwaka huu.

Akizungumza Afisa kilimo mazao manispaa ya Mpanda Gasto Mwakilembe amesema wataalamu wamejipanga vyema kuhakikisha wanatawasimamia vijana na kuwapa mafunzo ili waone tija katika kilimo biashara.

Back To Top