skip to Main Content

KATAVI.

Jamii mkoani Katavi imetakiwa kuondokana Na dhana potofu inayomkandamiza mwanamke kupata haki ya kumiliki mali, na badala yake kuwapa haki hiyo kama ilivyo kwa wanaume.

Wakizungumza Na mpanda redio fm baadhi ya wanawake mkoani hapa, wameeleza kuwa bado jamii imegubikwa na giza la mila potofu ya kutommilikisha mwanamke mali, jambo ambalo linawanyima fursa nyingi za kiuchumi na kuwarudisha nyuma katika maswala ya kiuzalishaji.

Nae Afisa maendeleo ya jamii ofisi ya mkuu wa mkoa wa Katavi Wilson Kenedy, ameeleza kuwa baadhi ya wanawake wanashindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa weledi, kutokana na changamoto iliyopo kwa baadhi ya jamii kushindwa kuwamilikisha mali ikiwemo ardhi.

Kwa upande wake Inspekta Kelvin Fuime kutoka kitengo cha polisi jamii Na dawati la jinsia Na Watoto mkoa wa Katavi,ameeleza kuwa kitendo cha kumnyima mwanamke fursa ya kujitafutia kipato, ni ukatili na unyanyasaji wa kijinsia huku akiwataka wanaume kuacha tabia ya mfumo dume.

Back To Top