Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imeshindwa kuendelea na ushahidi wa kesi ya Ugaidi na Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa sababu shahidi anaumwa.
Hayo yamebainishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando mbele ya Jaji Joachim Tiganga wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea na shahidi wa 6 wa Upande wa Jamhuri.
Aidha Wakili Kidando amesema “Shauri linakuja kwa ajili ya kusikilizwa, hadi jioni tulikuwa na shahidi ambaye alitakiwa kuja mahakamani ila amepata ugonjwa ambao umesababisha asije,
“Tunaomba ahirisho tuje na shahidi mwingine, hivyo ni sababu iliyo nje ya uwezo wetu.”