Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Baadhi ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu vilivyonufaika na mikopo ya asilimia 10 kutoka halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji, vimedaiwa kugawana fedha badala ya kuanzisha miradi ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zaidi ya shilingi milioni 100 kwa vikundi 17 vya Wanawake, Vijana na watu watu Wenye Ulemavu, afisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Kigoma Ujiji, Majira Jabili amesema tangu mikopo hiyo ianze kutolewa mwaka 2018, vikundi vitano vimegawana fedha.
Aidha mesema hali hiyo imesababisha kupotea kwa zaidi ya shilingi millioni 18, fedha ambazo ni za Serikali na ambazo zilitakiwa kurejeshwa na kukopeshwa kwa wahitaji wangine.