skip to Main Content

KATAVI

Wazazi mkoani katavi wameiomba serikali na wadau mbali mbali kusaidia upatikananji wa taulo za kike kwa wanafunzi waliopo mashuleni.

Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti tofauti walipokua wakizungumza na mpanda radio fm na kusema kuwa ili mwananfunzi wa kike kupata hedhi salama awapo shuleni ni wajibu wa kila mzazi,mlezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha kunakuwepo kwa mazingira rafiki ya kumuwezesha binti kusoma hata akiwa kipindi cha hedhi.

Beatrice Ghati ni afisa elimu watu wazima mkoani hapa ambae pia anahusika na  masuala ya afya mashuleni amesema kuwa wanaendelea kuboresha miundombinu ya afya bora kwa wasichana mashuleni ili kupata hedhi salama.

Tafiti zinaonesha kwamba kila siku wanawake zaidi ya milioni 12 wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wanakua kwenye hedhi duniani kote.

Back To Top