“Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wananchi wilayani humo kuacha kujihusisha na na…
“Wandishi wa habari Mkoani Katavi wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ili kuepusha sintofahamu kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025″. Picha na Ben Gadau
Na Ben Gadau-katavi
Wandishi wa habari Mkoani Katavi wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ili kuepusha sintofahamu kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Hayo yamezungumzwa na ACP David Mutasya kaimu kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Katika mdahalo wa nne baina ya waandishi wa habari , vyama vya siasa , viongozi wa dini na Jeshi la polisi mkoani hapa.
Walter Nguluchuma Mwenyekiti wa Waandishi wa habari Mkoani hapa amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya tasnia hiyo ili kuepukana na migogoro kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Pia Walter Mguluchuma Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Katavi ameushukuru Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC kwa kuona umuhimu wa kuwezesha midahalo hiyo kufanyika baina ya waandishi wa Habari na Jeshi la polisi.
Mguluchuma ametoa wito kwa waandishi wa habari mkoa wa Katavi kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao ili kuepusha migongano isiyokuwa ya lazima katika majukumu yao.
Picha ya washiriki wakisikiliza katika mdahalo huo, wadau, Waandishi Wa habari pamoja na jeshi la Polisi
Kwa upande wa washiriki wa mdahalo huo wametoa maoni mseto huku wakitaka pande zote kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na miiko inayo waongoza.
David Mutasya Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi kwa niaba ya kamanda wa Polisi mkoa mkoa wa Katavi amesema kuwa midahalo imekuwa na tija kubwa tangu ianze mwaka jana baina ya waandishi wa habari na jeshi la polisi katika mkoa wa Katavi.