skip to Main Content
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Kaster Ngonyani

Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi kupitia Misako limefanikiwa kukamata watuhumiwa 124 kwa makosa mbalimbali.

Na Gladness Richard – Katavi
Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi kupitia Misako iliyofanyika katika kipindi cha mwezi September 2023 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 124 kwa makosa mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi ACP Kaster Ngonyani amethibitisha kutokea kwa matukio hayo huku watuhumiwa kumi wakikamatwa wakiwa na mali mbalimbali za wizi walizoiba kwa kuvunja nyumba.

Ngonyani ameendelea kwa kusema kuwa kupitia mafanikio hayo na doria na misako,wamefanikiwa katika kesi mahakamani kwa watuhumiwa kuhukumiwa adhabu ya vifungo jela.

Wananchi wametakiwa kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika mapambano dhidi ya wahalifu kwa kutoa taarifa za wahalifu ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Back To Top