“Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wananchi wilayani humo kuacha kujihusisha na na…
Jeshi la polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wawili akiwemo Dotto Mathias (37) kwa tuhuma ya mauaji
Na Ben Gadau – Katavi
Jeshi la polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wawili akiwemo Dotto Mathias (37) kwa tuhuma ya mauaji yaliyotokea katika kitongoji cha kabatini kata ya mwese Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika.
Akizungumza kwa njia ya simu na Mpanda redio fm Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Kasta Ngonyani amesema tukio hilo limetokea October mwaka huu majira ya saa kumi jioni katika kitongoji hicho.
Aidha amewataja waliouawa kuwa ni Mariam Mtevu (13) na Esta Zubel Enock (2) huku akisema chanzo cha mauaji hayo ni baada ya mama wa Watoto hao kukataa kuwa na mahusiano na mmoja wa watuhumiwa hao.
Ngonyani ameendelea kuiasa jamii kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za matukio ya aina hiyo ikiwa ni sambamba na kutokomeza matukio hayo.