“Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wananchi wilayani humo kuacha kujihusisha na na…
MPANDA
Wananchi Mkoa wa Katavi wametoa maoni mseto juu ya ujio wa mradi wa umeme wa Grid ya Taifa kutoka Tabora kuja Mkoani Katavi.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm na kuongeza kuwa ujio wa umeme wa Grid ya Taifa utawasaidia kupunguza changamoto wanazopitia kwasasa na kupata umeme wa uhakika
Injinia Sospeter kutoka Shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Katavi amesema kuwa kazi inaendelea na kuwa hadi sasa wakandarasi wawili wako kazini ili kukamilisha zoezi hilo
Aidha Eng. Sospeter amesema kuwa tathmini ya malipo kwa wale watakao paswa kulipwa imeshafanyika na kuwa hadi kufikia mwisho wa mwaka huu umeme wa Grid ya Taifa utakuwa umefika Mkoani Katavi.