miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amemuagiza Mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda kuhakikisha ujenzi wa kituo cha afya kata ya Mwamkulu unakamilika ifikapo terehe 30 december 2022.
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi katika kituo hicho na kumuagiza mkurugenzi ifikapo january 2023 kituo hicho kianze kutoa huduma kwa wananchi ambao miaka 61 ya uhuru hawakuwa na kituo cha afya na wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kupata huduma za afya.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi Daktari wa Manispaa ya Mpanda Paul Swakala amesema kituo kina jumla ya majengo sita ikiwemo jengo la mama mtoto, jengo la upasuaji na jengo la kufulia, ambayo yote yapo zaidi ya asilimia 80 huku akiainisha changamoto za uchelewashwaji wa kukamilika kituo hicho ni kupata marighafi na kukosa ushirikiano kutoka kwa wananchi.
Kwa upande wao wananchi wa kata ya Mwamkulu wameeleza matamanio yao baada ya kukamilika kwa kituo hicho ambacho kwa muda mrefu ilikuwa shauku yao kupata huduma hiyo karibu yao.
Kituo hicho kinachojengwa kwa mfuko wa fedha za tozo kinagharimu takriban milio 500 huku kikitarajia kupunguza adha ya usumbufu kwa wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.