Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
TANGANYIKA.
Katika kuazimisha miaka 61 ya uhuru wa Tanzania bara wananchi wametakiwa kuziunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na viongozi ikiwa ni sehemu ya kumuenzi mwasisi baba wa taifa mwalimu Julius kambarage nyerere.
Kauli hiyo imetolewa na mgeni rasmi ambae ni mbunge mstaafu Hemed Sumry katika mdaharo wa kuazimisha miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Tanganyika ameeleza kuwa ili taifa lisonge mbele zaidi ni lazima uwepo mshikamano baina ya viongozi na wananchi.
Akiongelea mafanikio mbalimbali kwa sekta ya afya yaliyopatikana baada ya uhuru mganga mkuu wa wilaya ya Tanganyika Alex Mrema amesema kabla ya uhuru ilikuwa sio rahisi kila mtu kupata huduma ya afya ukilinganisha na sasa ambapo ameeleza kuwa miaka 61 ya uhuru sekta ya afya imeimarika kwa kuwa na hospitali za rufaa kila mkoa.
Siku ya uhuru wa Tanzania bara inaazimishwa na watanzania wote kila inapofika tarehe 09 ya mwezi wa 12 kila mwaka.