skip to Main Content

MPANDA
Mamlaka ya maji manispaa ya mpanda Ruwasa imeagizwa kuhakikisha mradi wa maji katika kata ya mwamkulu unakamilika ili kupunguza adha kwa wananchi.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph wakati akifanya ziara ya ukaguzi wa miradi katika kata hiyo amabayo kwa muda mrefu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata maji katika mito.

Awali diwani wa kata hiyo ya mwamkulu Kalipi Katani ameeleza changamoto zinazoikumba kata yake, ikiwemo changamoto ya maji na umeme na amemuomba mkuu wa wilaya kuzitatua changamoto hizo ili kuleta unafuu kwa wananchi na kurahishisha utendaji kazi katika kituo cha afya Mwamkulu.

Kwa upande wao wananchi wa kata ya Mwamkulu wameshukuru kuletewa mradi huo wa maji ambao umeanza kupunguza adha ya upatikanaji wa maji katika kata hiyo

Mradi huo ambao unagharimu shilingi milion 500 mpaka sasa upo katika zaidi ya asilimia 80 na tayari umeanza kutoa huduma kwa wananchi

Back To Top