skip to Main Content

TANGANYIKA.

Wananchi wa Kijiji cha Lugonesi Tarafa ya Mwese wilayani Tanganyika walionufaika na Fedha za mradi wa hewa ya ukaa, wameshukuru kuwepo kwa mradi huo, kwani umewawezesha kujenga zahanati kijijini hapo.

Wakizungumza mbele ya mkuu wa mkoa wa Katavi alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi katika Tarafa ya Mwese, wananchi  wamesema, uwepo wa zahanati hiyo utapunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Hata hivyo mkuu wa mkoa Katavi Mwananvua Mrindoko amemuagiza mkurugenzi wa wilaya ya Tanganyika, Shabani Juma baada ya miezi miwili zahanati hiyo ianze kutoa huduma kwa wananchi.

 Lakini pia mkuu wa Mkoa amemuagiza mkuu wa wilaya ya Tanganyika kufuatilia Tanesco ipeleke umeme wa REA kwa wakati, na kumtaka mkurugenzi anatafuta Sola ili huduma zianze kutolewa.

Aidha Mrindoko amewataka wananchi wa Lugonesi kuhakikisha wanaendelea kutunza maadhari ya Misitu kwa manufaa na maendeleo ya Kijiji, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Back To Top