skip to Main Content

KATAVI

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi Ali Makame Hamadi amewataka wananchi kuishi katika misingi na maadili ya dini ili kuondokana na matukio kiuhalifu.

Ameyasema hayo wakati akishiriki ibada katika kanisa la New harvest kijiji cha songambele Halmshauri ya Nsimbo amesema kuwa matukio mengi yanatokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na hofu ya Mungu huku akiendelea kuwataka wananchi kutoa taarifa zinzohusu matukio ya kiuhalifu.

Kwa upande wao baadhi ya waumini katika kanisa hilo wamepongeza baada ya kutembelewa na kamanda huyo huku wakiendelea kuomba zoezi hilo liwe endelevu katika kupambana na matukio ya kiuhalifu.

Back To Top