skip to Main Content

KATAVI

Wananchi Mkoani Katavi wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa Kusimamia ili kushusha bei ya Mahindi ambayo bado imeonekana kuwa kubwa kwa wananchi.

Wakizungumza na Mpanda Redio fm wananchi hao wamesema serikali isimamie kwa ukaribu juu ya kuangalia namna ya kushusha bei ya bidhaa hiyo ili kusaidia wananchi wenye hali ya chini.

Nao wafanyabiashara wamesema kuwa wanapanga bei ya mahindi na kuuza kwa bei hiyo kulingana na upatikanaji wa bidhaa hiyo na mahali walipochukulia.

Akizungumzia hali ya Uchumi katibu Tawala MSAIDIZI Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Katavi Bwana Nehemia James amesema kuwa Mwenendo wa Soko na Wafanya biashara ndiyo wapangao bei ya Bidhaa katika soko la uchumi huria nchini na wala si Serikali.

Back To Top