skip to Main Content

MPANDA

Diwani wa kata ya magamba ametoa siku mbili kwa Uongozi wa kikundi cha kagera group kuwasilisha taarifa ya uendeshaji wa kikundi hicho ili kurahisisha agenda ya uchaguzi kuziba nafasi za viongozi waliovuliwa nyadhifa zao.

Agizo hilo limetolewa na diwani wa kata ya Magamba Fortunatus Chiwanga wakati wa mkutano ambao uliwataka kuja na taarifa hiyo ili kufanya uchaguzi kwa nafasi za viongozi waliotenguliwa, ili kupata viongozi wapya katika kikundi hicho cha Kagera.

Akijibia hoja hiyo katibu mtendaji cha kikundi cha Kagera amesema kuwa watatekeleza agizo hilo kwa  muda waliopewa kwasilisha taarifa hiyo ili kutoa mwanga wa kikundi na jinsi gani viongozi wapya watapa sehemu ya kuanzia.

Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha dirifu wameuomba uongozi huo kukamilisha taarifa hiyo ili kumaliza mgogoro huo ili kupisha shughuli nyingine kuendelea.

Back To Top